Farida

Farida

Mke wa kwanza wa mzee Kizito. Bila shaka angekuwa mwanamke tofauti kama angekuwa kazaliwa karne ya 21. Lakini anatokana na nyakati ambapo wasichana walikuwa wakiolewa vijana sana na watoto wengi, akipika na kuwahudumia wengine bila kulalamika. Alipinga Kizito kuchukua mke wa pili, Mwanaidi; na alipooa mke wa tatu, Vingawaje, alijifunza kuchukia ushindani. Hata hivyo, si yeye ndiye alikuwa malkia wa Kizito? Na sasa ingawa anazeeka si wajibu wake kufurahia haki za mke mkubwa? Jaribu kumkiuka Farida halafu uone utakachokipata! Hamuogopi yeyote - Na ni rafiki ya mganga wa kienyeji, Mgongo.

ITV Siri ya Mtungi

Siri ya Mtungi Tafsiri

SYM Star Search